April 16 2017 katika uwanja wa Old Trafford Man United walicheza dhidi ya Chelsea katika muendelezo wa michezo yao ya Ligi Kuu England, upinzani mkubwa wa mchezo huu ulikuwa ni uwepo pia wa Jose Mourinho ndani ya Man United akishindana na timu yake ya zamani ya Chelsea kwa mara nyingine tena.
Katika mchezo huo Man United wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli yakifungwa na Marcus Rashford dakika ya 7 na Ander Herrera dakika ya 49, ushindi huo wa Man United dhidi ya Chelsea unakuwa ni ushindi wa kwanza toka waifunge Chelsea kwa mara ya mwisho October 28 2012.
sourcemillardayo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment