Mkenya Daniel Wanjiru ameshinda mbio za London Marathon na kumuacha mkali wa mbio hizo, Kenenisa Bekele akichukua nafasi ya pili.
Wanjiru raia wa Kenya ameshinda kwa muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 48 na kuonyesha alikuwa vizuri mbele ya Bekele.
Bekele ndiye anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za Mita 5000 na 10000 lakini hakuweza kufua dafu dhidi ya Mkenya huyo.
Kikubwa alichokuwa amelenga Wanjiru ni kuimaliza rekodi ya Mkenya mwenzake, Dennis Kimetto ya 2:02:57 lakini hata hivyo imeshindikana ingawa ameingia kwenye rekodi ya kuwa mmoja wa wanariadha bora kabisa kukimbia kwenye London Marathon.
Wanjiru na , mwishoni kulikuwa na ushindani mkali huku Bekele akionyesha kupunguza pengo dhidi ya Mkenya huyo, lakini mwisho Wanjiru alicharuka na kushinda,Mtanzania Alphonce Simbu yeye amemaliza katika nafasi ya tano katika mbio hizo za London Marathon
Kwa upande wa wanawake hii ni mara ya tatu kwa mkenya Mary Keitany kushinda London Marathon na kikubwa leo ameweka rekodi ya kukimbia kwa muda wa 2:17:01 ambayo ni rekodi mpya ya dunia.
Kutokana na ushindi huo, Mary anaondoka na kitita cha dola 125,000 (Sh milioni 273), kinachojumuisha uvunjaji wake wa rekodi hiyo.
Zawadi ya kawaida ya mshindi hula ni dola 55,000, lakini huongezeka kutokana na kuvunja rekodi.
Tirunesh Dibaba wa Ethiopia alifukuzana vikali na Mary Keitany katika dakika za mwisho hata hivyo Mkenya huyo alionyesha ni bora zaidi alipofanikiwa kuibuka na ushindi huo.
source:perfect255
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment