Monday, November 28, 2016

Mwakyembe ataka mahakimu 28 walioshinda kesi za rushwa wasirudishwe kazini

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe ameitaka tume ya utumishi wa mahakamana kutowarudisha kazini mahakimu 28 walioshinda kesi za rushwa zilizokuwa zikiwakabili kwa lengo la kulinda imani ya mahakama kwa wananchi badala yake mahakimu hao wafanye kazi nyingine.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe.
Waziri huyo ameyasema hayo katika ziara ya kiserikali ya siku 3 katika mikoa ya Mbeya na Songwe ambapo aliweza kutembelea ofisi ya msajili wa vizazi na vifo ambapo aliitaka ofisi hiyo na nyingine kuongeza kasi ya kusajili vizazi kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 ili kuiondolea Tanzania aibu.
“Kumekuwepo na watumishi wa mahakama ambao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za rushwa mahakamani, ambapo kati ya watumishi 30 wamekutwa na hatia na kufukuzwa kazi huku mahakimu wengine 28 wakishinda kesi zao. Lakini hawastahili kurejeshwa kazini waendelee kutoa haki kwa kuwa wananchi hawatakuwa na imani nao,” alisema Mwakyembe.
BY: EMMY MWAIPOPO

Source:bongo5

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video

0 comments:

Post a Comment