Miongoni mwa mchezo mkali jioni ya leo ni ule utakaowakutanisha Wanajangwani Yanga dhidi ya Wanarambaramba Azam FC mchezo utakaopigwa Jijini Dar es Salaam. Timu hizo zinashuka dimbani huku zikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo mmoja mmoja kwa kila timu baada ya kukubali kichapo kutoka kwa Stendi United ya Mkoani Shinyanga hivyo leo kila mmoja atashuka dimbani kujaribu kusawazisha makosa ya kupoteza mchezo huo.
Timu za Azam na Young Africans; zote za Dar es Salaam huku mwamuziki wa mchezo huo Na. 76 atakuwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam. Nkongo atasaidiwa na Soud Lila na Frank Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen Mduma; wote wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Michael Wambura pia wa Dar es Salaam.
Mchezo Na. 77 utazikutanisha timu za Ruvu Shooting na Mbeya City, kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Rudovic Charles wa Tabora akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jeremina Simon wa Dar es Salaam. Kamisha wa mchezo huo atakuwa Idelfonce Magali wa Morogoro.
Mtibwa Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya nazo zitacheza kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro. Mchezo huo Na. 78 utachezeshwa na Elly Sasii wa Dar es Salaam. Waamuzi wasaidizi ni Ferdinand Chacha wa Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa akiba Nicolaus Makalanga wa Morogoro. Kamishna ni George Komba wa Dodoma.
Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Toto African ya Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Mchezo huo Na. 79 utachezeshwa na mwamuzi Shomary Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah Uhako wa Arusha na Julius Kasitu wa Shinyanga huku mwamuzi wa akiba akiwa Mathew Akrama wa Mwanza. Kamishna atakuwa Michael Bundala wa Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment