Ernest Napoleon akiwa kwenye set ya filamu hiyo na Idris Sultan
Katika collabo zilizowahi kutikisa, Mzee wa Busara ya Juma Nature na Inspekta Haroun haiwezi kukosa kwenye 50 bora za muda wote.
Katika collabo zilizowahi kutikisa, Mzee wa Busara ya Juma Nature na Inspekta Haroun haiwezi kukosa kwenye 50 bora za muda wote.
Ni kwasababu ilikutanisha mahasimu hao wa Temeke kwa mara ya kwanza tangu kuwepo kwa bifu lao lililochagizwa na harakati za kila mmoja kuutetea ufalme wa TMK. Nguvu yake enzi hizo, ilikuwa ni sawa kama leo Diamond na Alikiba wafanye ngoma ya pamoja.
Na sasa, tarajia kuwasikia wakali hao kwenye ngoma nyingine, wakionesha umwamba wa Rap Katuni, na tena mpishi akiwa yule yule, Mdachi anayewawezea, P-Funk. Hiyo ni kwa hisani ya filamu ijayo, Karibu Kiumeni, inayochezwa na Ernest Napoleon.
“Ngoma zitakuwa kama sita, moja itakuwa Nature na Inspekta, watafanya ngoma itakayobeba jina la movie na maudhui ya Temeke,” Napoleon ameiambia Bongo5.
“Itakuwa ngoma ya kwanza ya kurap pamoja tokea Mzee wa Busara,” ameongeza.
Napo amesema kwenye soundtrack hiyo, TID atafanya ngoma na Adili huku Fid Q akifanya na AY.
Ameendelea kufafanua, “Damian Soul pia atafanya Ngoma ya mapenzi, halafu Msaga Sumu Sengeli. Wengine watakuwepo kama Young Killer, Dogo Janja, watafanya ngoma ya pamoja ya generation yao.”
Filamu hiyo imewakutanisha pia Idris Sultan, Irene Paul, Muhogo Mchungu, Rashid Matumla na wengine.
0 comments:
Post a Comment