Huwezi kuwataja wasanii wakali kibongobongo ukaacha kumtaja Barnaba Boy, ni mmoja kati ya wasanii wachache ambao wanaujua muziki kiundani kuanzia kwenye kuuimba hadi kwenye kuuandaa muziki wenyewe.
Lakini cha kushangaza ni kwamba hajawahi kusikika kwenye collabo ya kimataifa nje ya Afrika Mashariki ukiachana na ile “Nikutunze ambayo kafanya na Jose Chameleon wa Uganda.
Perfect255 ikaona haitakuwa vibaya kama ikimtafuta Barnaba na kujua kuna nini kati yake na collabo za kimataifa ukizingatia yeye ni msanii mkali. Ndipo kipaza cha Perfect255 kilipoweka kambi kwenye mdomo wa Barnaba Boy kwa dakika kadhaa baada ya kukutana backstage kwenye Fiesta ya Moshi.
“Kuhusu collabo za kimataifa muda ukifika kila kitu kitaenda sawa, na wala sijachelewa, kusikika kwenye collabo za international hakumaanishi wewe ni international” Ni maneno aliyoyazungumza Barnababaada ya kuulizwa kwanini hatumsikii kwenye collabo za kimataifa.
Barnaba pia ni mwalimu wa muziki, na wapo wasanii ambao wanafanya poa sana kwenye Bongo Fleva kwasasa ambao ni zao la Barnaba.
0 comments:
Post a Comment