Thursday, October 6, 2016

Simba imechagua uwanja itakaoutumia kwa mechi zake za nyumbani


Siku chache baada ya Yanga kuandika barua ya kuomba kuutumia uwanja wa Amaan Zanzibar kwa mechi zake za nyumbani, klabu ya Simba nayo imesema tayari imeshachagua uwanja utakaotumika kwa mechi zake za nyumbani.
Ofisa habari wa ‘Wekundu wa Msimbazi’ Haji Manara amesema, Simba tayari wameshachagua uwanja ambao watautumia kwa mechi zao za nyumbani lakini kwa sasa kipaumbele chao ni kuomba radhi kwa serikali ili kuruhusiwa kuutumia uwanja wa taifa, lakini kama wataendelea kuzuiliwa watautangaza uwanja huo waliouchagua.
“Simba tumeshachagua uwanja, lakini kwenye mchakato huu bado tunaendelea kuwaomba radhi Wizara. Kama alivyosema Rais wa nchi tunaamini wao ni wasikivu.”
“Kabla ya mechi yetu na Kagera Sugar ambayo tutacheza October 16 tunaamini suluhisho la jambo hili litakuwa limeshapatikana.”
“Uwanja huu hatuna haja ya kuutaja leo kwasababu sasahivi kipaumbele chetu ni kupiga magoti, yani ni sawa na umemkosea mzazi halafu wakati unamuomba msamaha unatafuta baba wa pembeni.”
“Itakapobidi, siku kadhaa kabla ya mechi yetu na Kagera tutautangaza lakini kwa sasa kipaumbele chetu kwenda kuomba radhi.”
Siku moja baada ya mchezo wa Yanga na Simba, Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh. Nape Nnauye alitangaza kuvipiga marufuku vilabu hivyo kuutumia uwanja wa taifa kutokana na uharibifu uliosababishwa na mashabiki wa timu hizo kwenye uwanja wa taifa.

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 

0 comments:

Post a Comment