Mi nilijua labda Chege kweli hayupo vizuri kwenye maswala ya ulinzi katika mtandao wake wa Instagram, Sasa Bad Newz ni kwamba rapper J cole naye amekuwa hacked katika akaunti yake ya twitter.
Mambo yamekuwa si mambo kwa rapper J Cole baada ya akaunti yake ya Tiwtter kuwa hacked na watu wasiojulikana, taarifa zinasema kwamba J cole hakuwahi kutumia kurasa yake ya twitter tangu mwezi wa tatu wa mwaka huu, mambo yamekuja kubadilika jana Oktoba 3 baada ya akaunti yake ya Twitter kuanza kutweet mambo ambayo yalikuwa yanashangaza kwa mashabiki kwa kuongelea situation ambayo ilimkuta Kim ya kuibiwa na mengine kibao.
Tukirudi nyumbani, wadukuzi wa hapa Bongo bado wanaendelea kuwatafuna wasanii wetu wa Bongofleva, Chege ni moja ya wasanii wa mwisho mwisho kukumbwa na mkasa huu wa kudukuliwa akaunti yake ya Instagram na mdukuzi huyo kuanza kuichezea akaunti ya chege anavyotaka yeye
0 comments:
Post a Comment