It’s official, baada ya kuonjesha kwa mafumbo picha yenye maneno ‘Juu’, Vanessa Mdee na Jux wamethibitisha kuwa ni wimbo wao wa pamoja.
Wawili hao wameshare kava la ngoma hiyo iliyotayarishwa na Lufa katika studio za Switch Records. “Kuna muda mi nashindwa kufanya vitu vingi kwako natamani kutimiza #Juu,” ameandika Vanessa kwenye Instagram katika picha ya kava hilo.
“Ila moyo unajua jinsi gani navyotaka kwenda sawa na wewe #Juu,” ameandika kwenye nyingine.
Naye Jux ameandika: Upendo wetu ndo muhimu kuwa pamoja mimi na wewe usije nipa wazimu kisa nakupenda we #JUU.”
Huo unakuwa wimbo wao wa kwanza kuutoa rasmi tangu wawe pamoja.
0 comments:
Post a Comment