Monday, October 17, 2016

KLITSCHKO KUPAMBANA NA JOSHUA

Bondia wa Uingereza Anthony Joshua na bondia wa Ukraine Wladmir Klitschko wamekubali kuzichapa huku tangazo la pigano hilo likitarajiwa kutolewa katika siku chache zijazo.

Kulingana na promota Eddie Hearn, pigano hilo la uzani mzito linafaa kuidhinishwa na ukanda wa Joshua wa IBF mbali na mikanda ya WBA naWBO.  Siku ya Jumatano bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury aliyaachia mataji yake ya WBO na WBA huku leseni yake ya kupigana ikifutiliwa mbali kwa muda.

Bodi ya Uingereza inayodhibiti leseni za mabondia ilimpokonya bondia huyo leseni yake kufuatia uchunguzi wa kutumia dawa za kuongeza nguvu, baada ya bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 kukiri kwamba amekuwa akitumia Cocaine ili kukabiliana na msongo wa mawazo.


By mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 




0 comments:

Post a Comment