Monday, October 17, 2016

Rais Magufuli aongoza mamia kumuaga Dk.Didas Masaburi, viwanja vya Karimjee Dar

Rais Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Dk.Didas Masaburi wakati kuaga mapema leo Jijini Dar eS alaam katika viwanja vya Karimjee.

Rais Magufuli ameongoza viongozi mbalimbali wa nchi na mamia waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Dk.Didas Masaburi wakati wa kuagwa mapema leo Jijini Dar eS alaam katika viwanja vya Karimjee.

MWILI wa Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, leo utaagwa na viongozi wa kitaifa pamoja wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Karimjee, kabla ya kwenda kuzikwa katika Chuo cha ugavi na ununuzi cha IPS kilichoko Chanika wilaya ya Ilala.

Msemaji wa familia, Edson Fungo alisema kuwa, kwa kuwa Dk Masaburi alikuwa mwanasiasa na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikalini, familia imeona vyema watoe fursa ya kuagwa na wanasiasa wenzake pamoja na wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Dk Masaburi kabla ya kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Wakati akiwa Meya alichaguliwa pia kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALART).

Hadi mauti yanamkuta, Dk Masaburi alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Chuo cha IPS kilichoko Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Ni katika eneo la chuo hicho ndiko marehemu atazikwa leo. Ratiba iliyotolewa na Msemaji huyo wa familia hiyo, inaonesha kuwa saa 3.00 mwili ndio utawasili kwenye Ukumbi wa Karimjee na ibada itaanza saa 4.00 asubuhi.

Utasomwa wasifu wa marehemu na baadaye kutakuwa na neno kutoka kwenye Chama Cha Mapinduzi na viongozi wa serikali.

Shughuli ya kuaga mwili wa marehemu itaanza saa 5.00 na saa 6.30 mchana msafara kwenda Chanika utaanza. Utakapowasili kutafanyika ibada ya maziko na pia wananchi wa maeneo hayo na wanajumuiya ya IPS wataanza kuaga.



Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 





0 comments:

Post a Comment