Monday, October 17, 2016

TANZANIA HATUTAPOKEA MISAADA YENYE MASHARTI MAGUMU : SAMIA


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema wakati umefika wa Tanzania kujitegemea kiuchumi, na kwamba, nchi haiko tayari kupokea misaada yenye masharti, ambayo hayaendani na mila na desturi zetu.

“Hatukubali kupokea misaada ambayo ina masharti magumu, tubadilike na tuendelee kuijenga Tanzania yetu, twendeni kwa mtindo wa kuijenga Tanzania yetu, tubane matumizi, tukusanye mapato,” alisema Makamu wa Rais jana wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya wakazi wa Dodoma.

Makamu wa Rais alisema wakati umefika kwa Tanzania kujitegemea, japo haijafika asilimia 100 ya kujitegemea angalau iko asilimia 60.

“Tunasema tunaendesha serikali hii kwa mapato yetu ya ndani. Mapato ya nje tumetumia kwa miaka mingi nadhani sasa hivi wanaona Tanzania tumetumia mapato yao muda mrefu kwa hiyo sasa wanakuja na kivuli cha kutupa masharti, mengine yako magumu kwa mila na desturi zetu hayatekelezeki na tunaposema hatutaki wanasema tunatoa fedha kwenye eneo lile wanatutishia kwenye eneo la ARV kwani wanajua tukikataa ndugu zetu watapukutika na wanaona tukiwabana hapa watakubali,” alisema.

“Tumeanza kurekebisha sheria ya manunuzi angalau sio njia hii wapita njia ile ili wafanye manunuzi,” alisema Makamu wa Rais. Aliongeza kuwa kuna mapungufu ya mapato kwenye halmashauri nchini kutokana na sababu za kutokusanywa au zikikusanywa zinaliwa.


By mtembezi 

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 

0 comments:

Post a Comment