Friday, October 7, 2016

DIAMOND KUTUMBUIZA KWENYE ZIARA YA UINGEREZA YA STAA HUYU WA MAREKANI

Muimbaji wa ‘Salome’ Diamond Platnumz ataungana na staa wa Marekani na mshindi wa Grammy, Neyo kwenye ziara ya pamoja mwezi disemba mwaka huu.
Diamond na Neyo ambao pia wameshirikiana kwenye wimbo ambao bado haujatoka ‘Marry you’ watatumbuiza pamoja kwenye show sita ya miji mbalimbali ya Uingereza.

Taarifa hizi zimetolewa na Revolt Africa, “Africa & America join forces!! @DiamondPlatnumz & @Neyo UK tour this December! The movement continues…” Wameandika  kwenye page yao ya Instagram“#AfricaToTheWorld #MusicToTheWorld #Neyo #neyonation #diamondplatnumz #rnbking #rnb #Tanzania #africa #afropop #afrornb #afrobeatsuk #afrobeats #afrobeat #kidogo #wcb #revolttvafrica #afroBeHeard,”
Hivi karibuni Diamond pia aliasema kuwa kuna kitu kikubwa atafanya na Neyo mwezi disemba mwaka huu.


0 comments:

Post a Comment