Thursday, September 29, 2016

JAY MO: ‘TUSIDHARAU PESA NDOGO TUKITEGEMEA KUBWA’


Rapa Jay Mo ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Pesa Madafu’ amefunguka na kusema kuwa Watanzania hususani vijana wamekuwa na tabia ya kudharua pesa fulani ndogo au ambayo haina thamani nakutegemea kupata pesa kubwa zaidi


Jay MO alisema haya kupitia kipindi cha ‘Ngaz kwa Ngaz’ kinachorushwa na EATV na kudai kuwa kumekuwa na vijana wengi ambao
wamekosa kazi au wameacha kazi kwa matarajio ya kupata kazi ambazo zinaweza kuwaingizia pesa nyingi.
“Pesa madafu ni pesa ambayo haina thamani kubwa inaweza kuwa dollar ila dollar moja bado haina thamani sababu haiwezi kufanya mambo makubwa, na sisi Watanzania tunahiyo tabia siku hizi ya kudharau pesa fulani ambazo hazina thamani kubwa ‘especialy’ sisi vijana nimeona watu wengi unakuta wana degree lakini tupo nao mtaani nikimuuliza vipi kuhusu kazi anakwambia pale mimi nimeacha kwa sababu mshahara mdogo”. Amesema
Mo ameendelea kufunguka kwa kutoa haya kama ushauri:
“Jamani hizi hizi pesa ndogo tusizidharau
tukikaa tu ili kusubiri pesa nyingi zije tununue Costa au mabasi zinaweza zisije kabisa, kwa hiyo tuzichange hizi hizi ndogo na wewe mwenye degree ukisikiliza ‘Pesa madafu’ inaweza kuku encourage na kusababisha uje kulipwa mshahara
mkubwa” alisema Jay Mo

0 comments:

Post a Comment