Wednesday, September 21, 2016

BATULI AITETEA BONGO MOVIE, ASEMA HAIJAFA KAMA WATU WANAVYODAI




Kuna wakati ambapo kila mtu huwa na lake la kusema katika kuongelea jambo linalogusa maslahi yake.
Kama mwanadada msanii mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ anayepingana na kauli ambazo hutolewa na baadhi ya wasanii kuwa
tasnia ya filamu imeshuka au inaelekea
kaburini.

Akipiga story na filamu central Batuli aliweza kufunguka haya..



“Huwezi kubishana na mtu kuhusu kusema kuwa Bongo Movie imeshuka au imekufa ni mtazamo wa mtu lakini kwangu naona ipo hai na watu tunaendelea kufanya kazi kama kawaida na watu wanapata riziki kwa kifupi Bongo Movie haijafa,”alisema Batuli.
Batuli anasema kuwa “Ni vema watu kufanya
utafiti na kuboresha sehemu zenye matatizo na sio kuwakatisha tamaa kwani bado wanao wapenzi wengi wa kazi zao na wanawakubali kupitia filamu na si kitu kingine”.
“Ukiona msanii anafanya biashara nyingine ni katika kujiongezea kipato kutokana na mfumo uliopo”. Aliongezea Batuli.

0 comments:

Post a Comment