Wednesday, September 21, 2016

DULLY SYKES ASEMA HAWEZI KUACHA KAZI HII KWAKUWA HAKUSOMA


Msanii Dully Sykes ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Inde’ amefunguka na kusema kuwa yeye atakufa kwenye muziki kwani hawezi kuacha kufanya muziki kwa kuwa muziki ndiyo maisha yake.
Akiongea kwenye Planet Bongo Dully Sykes amesema kuwa yeye hakusoma shule hivyo hawezi kusema anaacha muziki au kustaafu muziki bali yeye atakomaa na muziki
mpaka siku yake ya mwisho katika dunia hii.




“Mimi siyo kama Fid Q yule amesoma hivyo
anaweza kusema aache muziki akafanya kitu
kingine alichosomea sasa mimi shule sikwenda mimi nitafanya muziki kwani maisha yangu mimi ni muziki, muziki ni kazi yangu, naendesha maisha yangu na familia yangu kwa sababu ya muziki, na kama ningetaka kufanya kitu kingine
nadhani ningekuwa nimeshakata tamaa na muziki lakini mimi na muziki ni kama nimesomea darasani, baba yangu mwenyewe amekufa anafanya muziki na mimi nitakufa nafanya muziki siwezi kuacha” alisema Dully Skyes.
Mbali na hilo Dully Skyes amesema kuwa kwa sasa hafikiri kutoa albam kwani haamini kama inaweza kuwa biashara labda mpaka aone kuna msanii ametoa albam na amefaidika na mauzo ndiyo yeye anaweza kuja kutoa albam.
“Mimi sitaki kujaribu suala la albam kwani kwa upande wangu sioni kama ni biashara kwa sasa ila wakati mimi naanza muziki uongo albam ilikuwa biashara kweli, nikitoa leo albam nikija kutambulisha tu hapa nikitoka nje hapo tayari itakuwa imeshazagaa.
Kipindi chetu albam zilikuwa zinalipa sana na tumefaidika sana ila akitokea saizi mtu akatoa albam na akasema
imemlipa hapo ndiyo nitawaza ila mimi siwezi kujaribu kutoa albam saizi” alisema Dully Skyes

0 comments:

Post a Comment