Baada ya jana June 5 2017 kuchezwa michezo ya ufunguzi wa michuano ya SportPesa Super Cup 2017 na kushuhudia AFC Leopards ya Kenya na Yanga ya Tanzania zikifuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup.
Leo June 6 2017 michezo ya robo fainali miwili ilichezwa katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, mchezo wa kwanza ulikuwa Gor Mahia dhidi ya Jang’ombe Boys ya Kenya wakati mchezo wa pili ulikuwa wa Simba dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya.
Ushindi wa magoli 2-0 wa Gor Mahia umeipeleka Gor Mahia nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup na sasa walikuwa wanamsubiri mshindi wa mchezo dhidi ya Simba na Nakuru kujua watacheza na nani nusu fainali.
Wekundu wa Msimbazi Simba wamejikuta wakiaga michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kufungwa na Nakuru All Stars kwa mikwaju ya penati 5-4, hiyo ni baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare tasa na golikipa wa Simba Daniel Agyei ndio alikosa penati katika mchezo huo, hivyo Gor Mahia atacheza na Nakuru nusu fainali ya pilia.
source:millardayo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment