Baada ya kumuapisha, moja ya vitu alivizungumza Rais JPM ni kuhusu ile kauli yake ya kutoteua upinzani… kauli ambayo imekua ikisambaa kwenye video fupi baada ya kumteua Mama Anna Mghwira.
Leo Ikulu Rais Magufuli amesema ‘Siku zote nimekua nikisisitiza Tanzania kwanza, wapo wengine wanasema mbona ulishazungumza kuwa hutoteua upinzani? lazima watu waelewe nilizungumza hilo mahali gani…… nilizungumza hilo nikiwa Zanzibar‘
‘Pia msimamo wa kutoteua Mbunge wa Upinzani katika nafasi zangu 10 sitafanya hivyo kweli, nimeshateua 9 nimebakiza nafasi moja na hiyo nafasi moja haitokua ya Wapinzani’
JPM alimwambia Mama Mghwira ‘Wapo watakaokuonea wivu wa kwenye chama chako, wapo watakaokuonea wivu ambao walitaka nichague tu kutoka CCM‘
‘Wapo watakaokuonea wivu hata wa CHADEMA sababu sikuchagua huko pamoja na kwamba wapo wengi wananiombaomba, mpaka Wabunge lakini nimesema hapana… nataka upinzani uwepo‘ – Rais Magufuli
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment