Tuesday, June 6, 2017

Magufuli amwapisha Anna Mghwira kuongoza mkoa wa Kilimanjaro

Rais Dk John Magufuli amemwapisha Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam mapema leo.

Kiapo hicho kinafuatia uteuzi alioufanya Rais Magufuli kwa Mwenyekiti huyo wa chama cha ACT – Wazalendo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mapema mwezi huu.
Mara baada ya kiapo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira alipanda gari lake la kazini na kuelekea Mkoani Kilimanjaro kuanza kazi rasmi. Mama Anna Mghwira anachukua nafasi ya Said Meck Sadiq ambaye aliomba kujiuzulu na kukubaliwa na Rais Dk John Magufuli.

Mkoa wa Kilimanjaro umepata kuongozwa na wakuu wa mkoa watatu katika kipindi cha miaka miwili, Leonidas Gama ambaye ni mbunge wa Songea Mjini, Said Meck Sadick na Anna Elisha Mghwira.

Mghwira ameapishwa leo na tayari amekabidhiwa ilani ya CCM

Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment