Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema serikali inaendelea kupitia sheria, kanuni na taratibu za misamaha ya kodi mwaka hadi mwaka ili kuhakikisha kuwa misamaha yote isiyokuwa na tija inafutwa na hivyo kuiwezesha Serikali kuongeza mapato.
Hayo yamezungumzwa Bungeni mjini Dodoma na Dkt Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Masasi, Mhe. Rashid Chuachua (CCM), lililohoji namna gani serikali inavyodhibiti misamaha ya kodi tangu irekodiwe kwa viwango vya juu Mwaka wa Fedha 2011/2012.
Akijibu swali hilo Dkt Kijaji,alisema misamaha ya kodi kama sehemu ya asilimia ya Pato la Taifa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013/14 hadi sasa imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka. Misamaha hiyo ilikuwa asilimia 2.2 ya Pato la Taifa mwaka 2013/14, asilimia 1.9 ya Pato la Taifa, katika mwaka 2014/15 na asilimia 1.1 ya Pato la Taifa katika mwaka 2015/16” Alifafanua Dkt. Kijaji.
“Misamaha ya kodi ikilinganishwa na mapato ya kodi imekuwa ikipungua kutoka asilimia 18 ya mwaka 2013/2014 hadi kufikia asilimia 8.6 ya mapato yote ya kodi katika mwaka 2015-2016.”
“Misamaha ya kodi inatolewa na Serikali kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kodi zilizopo, huku kukiwa na baadhi ya huduma zinazotolewa katika jamii ambazo hazistahili kulipiwa kodi kwa sababu hazina manufaa ya kibiashara. Pamoja na hatua nzuri zinazochukuliwa na Serikali za kupunguza misamaha ya kodi ni vema ikafahamika kwamba si kila msamaha wa kodi una madhara hasi katika jamii na uchumi kwa ujumla,” Alisema Dkt Kijaju.
Na Emmy Mwaipopo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment