Monday, May 8, 2017

Serengeti Boys imetuma salamu za pole kwa watanzania

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ Bakari Shime ametuma salamu za rambirambi kwa watanzania wote kufuatia vifo vya wanafunzi wa shule ya msingi St. Lucky Vicent na watu wengine watatu wakiwemo walimu na dereva.
“Nitoe pole kwa watanzania wote kwa ujumla kwa niaba ya Serengeti Boys, sisi tumeguswa sana na tukio la ajali lililotokea kule Karatu, Arusha.”
“Taarifa hii ni ya huzuni sana lakini mwisho wa siku Mungu ndiye amepanga. Lakini kwa niaba ya benchi la ufundi na wachezaji wote wa Serengeti Boys nitoe pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkuu wa mkoa wa Arusha, familia, ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.”
“Timu imefika salama Gabon na tayari tupo kwenye uwanja wa vita na tuko tayari kwa vita ambayo ipo mbele yetu, leo tutaanza mazoezi mepesi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa kwanza siku ya Jumatano dhidi ya Mali.”
Mei 6, 2017 ilitokea ajali kwenye mlima wa Rhota, Karatu, Arusha iliyohusisha basi dogo lililobeba wanafunzi  waliokuwa wanakwenda kwenye mtihani wa ujirani mwema katika shule ya msingi Karatu.
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment