Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema hawezi kulifumbia mambo jambo la watu kutekwa na watu wasiojulikana.
Bashe ameyaanisha hayo Jumatatu hii na kusema kuwa na yeye ni mmoja wa watu wa waliotumiwa ujumbe wa vitisho ambao ulisema atafanyiwa vitendo vibaya popote alipo.
“Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana. Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo,” ameandika mbunge huyo kupitia akaunti yake ya Twitter.
Na Emmy Mwaipopo
Source:millardayo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment