Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameendelea kuzungumzia na kusisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada kwa eneo litakalokumbwa na njaa huku akisisitiza kulima mazao ya chakula kwakuwa mvua zinanyesha.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Alhamis wakati akizungumza na wananchi wa Somanga, Nangurukuru na Mchinga Moja ya ziara yake ya siku nne katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
“Kwahiyo naomba niwaombe ndugu zangu wa Somanga, mvua zimeanza kunyesha majani yameanza kuota, tuitumie ardhi hii na mvua hii kulima, tulime kila kitu ili kusudi tusije siku nyingine tuanze kulalamika njaa. Tumezoea kuambiwa maneno matamu kwamba hakuna mtu atakayekufa na njaa, mimi nawaambia msipolima mtakufa na njaa, usipofanya kazi utakufa na njaa. Ni lazima niwaambie ukweli, mlinichagua niwaambie ukweli, hizi mvua zinazonyesha ndugu zangu wa Somanga tuzitumie katika kulima na nina uhakika katika haya tutajenga uchumi wetu.”
Rais Magufuli anaendelea na ziara yake Ijumaa hii Mkoani Lindi.
0 comments:
Post a Comment