Saturday, March 4, 2017

Jokate afunguka hivi baada ya kuulizwa.......

Kila staa ana namna anawaangalia viongozi wa nchi pamoja na wadau kutoka katika nyanja mbalimbali.
Jokate alipata fursa ya kuwazungumzia baadhi ya viongozi pamoja na wasanii na kutoa mtazamo wake jinsi anavyowachukulia.
Mwanamitindo huyo akiwa katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Jumamosi hii aliulizwa swali ‘Nini kinakujia kwa haraka unaposikia jina Rais Magufuli, RC Makonda, Zitto Kabwe, Alikiba pamoja na Diamond Platnumz”.
Akijibu swahi hilo Jokate alisema, “Namfahamu Zitto Kabwe kama mtu smart sana, ukitaja jina la Mh Paul Makonda inanijia picha ya “Mbabe wa Vita” . Ukitaja Alikiba inanijia picha ya muimbaji mzuri. Ukitaja Diamond Platnumz namuona mtu mchapakazi (anajituma sana ). Kuhusu Rais Dr John Pombe Magufuli namuelezea kama TingaTinga ( mtu wa kazi ) , Mh Rais yuko vizuri sana,” alisema Jokate.


0 comments:

Post a Comment