Saturday, March 4, 2017

Mama Salma Kikwete afunguka baada ya kuteuliwa kuwa mbunge

Mke wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Salma Kikwete, amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumwona na kumteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mama Salma pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM akitokea Wilaya ya Lindi Mjini. Alitoa shukrani hizo wakati alipopewa nafasi ya kutoa salamu kwa wakazi wa Kata ya Nga’pa waliohudhuria ziara ya Rais Magufuli ya kukagua mradi wa maji wa eneo hilo.
Mama Salma alijitokeza Ijumaa hii katika ziara ya Rais Dk. Magufuli mkoani humo ambapo mbali na kutoa shukrani hizo alisema tatizo la maji katika Manispaa ya Lindi limekuwa kero ambayo inanyima utulivu kwa watendaji na viongozi wa wilaya na mkoa huo kwa ujumla.
Aidha Mama Salma alisema kwa nafasi aliyopewa atahakikisha anawawakilisha vyema wananchi wa Lindi na atashirikiana na wabunge wa mkoa huo kutatua kero ya maji.
By: Emmy Mwaipopo

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment