Hivi karibuni Mama wa mwimbaji wa BongoFleva, Alikiba alidai kuwa anamchukulia Jokate kama rafiki wa Zabibu “dada wa Alikiba” na kuhusu kuwa rafiki wa Alikiba hajui kwani hajatambulishwa. Alikiba naye alipoulizwa alidai Jokate si mpenzi wake bali rafiki yake tu.
Leo March 4 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV Mrembo Jokate ameulizwa anachukulia vipi hayo majibu yaliyotolewa na Mama yake Alikiba na Alikiba mwenyewe.
Haya ni majibu yake…..>>> “Unajua katika maisha huwezi kumlazimisha mtu kuona thamani yako, wanasema tenda wema nenda zako mengine ni matokeo na sipendi kulizungumzia sana maana siku hizi watu wanapenda sana kuokota maneno wanayatengeneza wanavyojua wao”
>>>”Mimi sifikirii sana maana mimi ni mtu Positive nataka niamini hawakuamaanisha sasa sijui waliteleza au walikosea”
0 comments:
Post a Comment