Thursday, March 2, 2017

Ridhiwan amwandikia ujumbe huu Mama Salma Kikwete baada ya kuteuliwa kuwa mbunge

Mbunge wa Jimbo la Chalinze na mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Ridhiwani Kikwete amemuandikia ujumbe wa pongezi mama yake Mama Salma Kikwete kuonesha amefurahia mama yake kuteuliwa kuwa mbunge.
Ridhiwani ameyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram:
“Umekuwa mtetea wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia, umewezesha wasichana kupata elimu.Wewe ni Mwanamke wa Shoka.Hongera sana kwa uteuzi‬. Imani sasa umepata sehemu ya kuwezesha mapambano kuwa sheria. Mungu akutangulie Mama yangu , Mheshimiwa Mbunge. Hongera tena.”
Mama Salma Kikwete ameteuliwa kuwa mbunge jana na Rais Magufuli.
By: Emmy Mwaipopo


Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment