Monday, February 20, 2017

ujumbe wa Shamsa Ford kwa mumewe Chidi Mapenzi

Japo Shamsa Ford anaonekana kupitia katika kipindi kigumu baada ya mumewe Rashidi Saidi aka Chidi Mapenzi jina lake kuwepo katika orodha ya watu wanaodaiwa kuhusika na madawa ya kulevya, muigizaji huyo ameonekana kusimama imara huku akimtia moyo.
Kupitia mtandao wa Instagram, Shamsa ameandika:
nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya. Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani inshaallah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..
Hata hivyo Chidi anatarajiwa kupandishwa kizimbani Jumatatu hii katika mahakama ya Kisutu.


0 comments:

Post a Comment