Wednesday, February 8, 2017

Mbowe, Gwajima, Idd Azan, Manji watajwa kwenye orodha ya pili ya Makonda

Mbunge wa Hai Freeman Aikaely Mbowe, mfanyabiashara mkubwa nchini, Yusuf Manji na Mchungaji Josephat Gwajima wametajwa kwenye orodha ya pili ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya watu mashuhuri wanaohusishwa kwenye biashara ya madawa ya kulevya.
Makonda amemtaja pia mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azan na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein Pambakali kwenye orodha hiyo.
Ameielezea orodha hiyo kuwa ni ya wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo.
Watu hao watahojiwa na polisi kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya kwanza iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu.
Wengine wanaohitaji ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club.
Orodha ya awamu ya pili ya Makonda ina jumla ya majina 65.

0 comments:

Post a Comment