Friday, February 17, 2017

ALIKIBA AKABIDHIWA TUZO YA MTV EMA BEST AFRICAN ACT

Ilikuwa mwishoni mwa mwaka jana ndipo ambapo Mnigeria Wizkid alipotangazwa kimakosa kama mshindi wa Best African Act katika tuzo za MTV Europe Music Awards ikiwa mshindi halali wa tuzo hiyo ni Mtanzania Alikiba.
Ndipo ambapo uongozi wa msanii Alikiba ulipoamua kuchukua hatua na kuhakikisha tuzo hiyo inarudi kwao ikiwa wao ndio washindi halali wa tuzo hiyo.
Siku chache baadae MTV walikiri kuitoa tuzo hiyo kimakosa na kuahidi hatua zitachukuliwa kuhakikisha tuzo inarudi kwa mshindi sahihi.
Hatimaye Alikiba amekabidhiwa tuzo hiyo mapema leo hii, kupitia twitter account ya MTV Base East wametusanua mchongo huo.

Alikiba na tuzo yake ya MTV EMA
Kila la kheri kwa mwana Bongo Fleva Alikiba katika harakati za kuipeperusha bendera ya Tanzania kila kona ya Dunia.

0 comments:

Post a Comment