Chura wa Snura unaweza ukawa ndio wimbo uliowahi kumpa misukosuko zaidi kwenye maisha yake ya muziki, lakini so far ndio wimbo wake uliofika mbali kuliko zote alizowahi kuzitoa.
Miongoni mwa sehemu ambazo Chura iliyabariki masikio ya wengi, ni Nigeria ambako clip zinazoonesha wanawake wakikata viuno kwenye wimbo huo zilikuwa viral.
Mmoja wa watu mashuhuri ambao bado wanaukubali wimbo huo, ni CEO wa Mavin Records, producer tajiri wa nchini humo, Don Jazzy. supastaa huyo ameshare kipande kifupi cha video akiimba wimbo huo kwa ufundi.
“Lol TZ did I get it right? #255 #Chura ,” ameandika staa huyo ambaye jina lake halisi ni Michael Collins Ajereh.
Mashabiki wake wa Tanzania wamemsifia kuwa amepita mule mule.
Source:bongo5
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
0 comments:
Post a Comment