
Meneja
wa TANROADS mkoa wa Shinyanga Mhandisi Wittonde Philipo ameelezea
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara mkoani mwake na kueleza
kwamba maendeleo ya miradi mkoani mwake ni mazuri.
Akiongea na
Afisa habari wa TANROADS Bi. Aisha Malima, Mhandisi Phillipo alisema
kuwa miradi miwili ipo katika hatua za kati na mwisho katika utekelezaji
wake.
Miongoni mwa
miradi iliyotembelewa na Afisa Habari huyo na ujumbe wake ni barabara
ya Mwigumbi – Maswa yenye kilometa 50.30 inayounganisha mkoa wa
Shinyanga na Simiyu.Kwa upande wa mkoa wa Shinyanga ni kilometa 16 na
kilometa 34 mkoa wa Simiyu.

Meneja wa
Mkoa wa TANROADS Shinyanga (katikati) akipewa maelezo juu ya ujenzi wa
Barabara ya Mwigumbi – Maswa (km 50.30) na Mhandisi Mshauri wa Kampuni
ya Kikandarasi ya KYONGDONG Engineering Co. Ltd ndugu Kim Hyung Gyu
Mradi huu
umeanza mwaka jana mwezi wa sita na matarajio ni kumaliza Aprili mwaka
ujao. Utekelezaji wa mradi huu ambapo kwa sasa ni asilimia 65
unasimamiwa na Kampuni ya Mkandarasi ya CHICO kutoka China pamoja na
Wahandisi Washauri wa Kampuni ya KYONDONG Engineering Co. Ltd kutoka
Korea ya Kusini, JV CORE Consulting PLC ya Ethopia, LUPTA Consults Ltd
ya Tanzania na ACE Consultants kwa gharama ya shilling billioni 61.461
na inafadhiliwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Tanzania.
Mhandisi
Wittonde Phillipo alielezea changamoto kadha zilizojitokeza wakati wa
ujenzi wa barabara hizo kuwa ni ukosefu wa maji kwa ajili ya kazi ya
ujenzi. Aidha wakati wa masika mkandarasi aliweka jitihada ya kuchimba
mabwawa kuhakikisha kazi haisimami kutokana na ukosefu wa maji.

Kazi za ujenzi katika barabara ya Mwigumbi – Maswa (km 50.30) zikiendelea.
Changamoto
nyingine ilikuwa eneo la kujenga barabara ambapo alitumia fursa
kuwashukuru wananchi walio toa ushirikiano wa kutosha na walio vunja
nyumba zao bila ya matatizo yeyote.
Mhandisi
Phillipo alieleza kwamba barabara hii inaendelea vizuri na kwa sasa mkoa
wa Shinyanga una miradi mingi ambayo imekamilika kwa kiwango cha lami .
Ujumbe huo
ulimaliza ziara yake kwa kutembelea mradi wa barabara ya mkoa ya Uhuru
ambayo iko eneo la Lubaga inayojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia
mia moja. Barabara hii ya katikati ya mji itakuwa na upana wa mita
6.5 na sehemu ya watembea kwa miguu na waendesha pikipiki ya miguu
miwili na mitatu.

Barabara hii
inajengwa na Mkandarasi mzawa JOTAN Engineering ikiwa ni mkakati
mojawapo iliyowekwa kuhakikisha nao wakandarasi wazawa wanapewa nafasi
katika miradi ya ujenzi wa barabara.
Afisa Habari
huyo wa TANROADS alitoa wito kwa wananchi watunze barabara ambazo
zinajengewa kwa pesa ya kodi za wananchi na kuomba madereva wahakikishe
hawazidishi uzito katika magari kwa lengo la kulinda barabara ziweze
kudumu kwa muda uliopangwa.
Alimaliza kwa
kusema kwamba alama za barabarani pia zina umuhimu mkubwa na
zinaitajika pia kulindwa ili kunusuru maisha ya watu na mali zao kwani
zikikosekana zinaweza kusababisha ajali.
Afisa Habari
huyo alimtembelea Mhandisi wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga katika ziara ya
kikazi iliyolenga kupata habari za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa
barabara mkoani humo.



Ndugu Kim Hyung Gyu – Mhandisi Mshauri akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo ya kitaifa wa Mwigumbi – Maswa (km 50.30) kwa Meneja wa Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Augustino Wittonde Phillipo.

Meneja wa
Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Augustino Wittonde Phillipo akikagua culvert
la dharura yanayo tumika wakati barabara inapokatika kutokana mafuriko
kulia ni Afisa Habari Mkuu wa TANROADS Bi. Aisha Malima.
0 comments:
Post a Comment