Monday, December 12, 2016

MELI ILIYOBEBA MALORI YA DANGOTE YAACHA HISTORIA MTWARA

Shehena ya malori 651 kwa ajili ya kusafirisha saruji kutoka kiwanda cha bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote imeweka rekodi ya meli kubwa kuwahi kutia nanga katika Bandari ya Mtwara.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dk Khatibu Kazungu alisema kwa mara ya kwanza meli kubwa ijulikanayo Morning Composer imetia nanga na kushusha malori 651 katika bandari hiyo.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya magari hayo bandarini hapo jana, Dk Kazungu alisema kufika kwa meli hiyo kutoka mashariki ya mbali kumefungua fursa za kiuchumi Mtwara na kuitangazia dunia kwamba bandari hiyo ina uwezo kama zilivyo nyingine duniani.


Source:mtembezi
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video




0 comments:

Post a Comment