Saturday, December 3, 2016

Majaliwa aitaka idara ya uhamiaji kuthibiti uhamiaji haramu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameitaka idara ya uhamiaji kudhibiti wahamiaji haramu huku ikianza misako katika nyumba za kulala wageni ili kubaini wanaoingia nchini bila vibali na kwamba anataka taarifa za wageni hao.


Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na walimu wa halmashauri ya Jiji la Arusha na wilaya ya Arusha kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Arusha. Ameitaka mikoa yote iliyopo mipakani kuhimarisha ulinzi kuthibiti wahamiaji haramu.
Hata hivyo Waziri Majaliwa amesema kuwa ni lazima idara ya uhamiaji ihakikishe inathibiti uhamiaji haramu kutoka sehemu mbalimbali za nchi alisema huku akisema kuwa, “leo hii tunafikia milioni 51 tukiwa zaidi nchi hii itakuwa na watu milioni 60 serikali itashindwa kutoa huduma kwa watu wake kwa mujibu wa bajeti yake kwa mujibu wa sensa tutaanza kulaumiana hapa kumbe kuna mzigo wa kuwahudumia watu ambao si wetu.”
Aidha Majaliwa aliongeza, “hatukatazi wageni kutoka mataifa mengine kutoka nchini ila lazima uthibiti wa wageni hao ufanyike ikiwa ni pamoja na kujiridhisha sababu za kuja nchini na muda watakao kuwepo.”
BY: EMMY MWAIPOPO

Source:bongo5

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video

0 comments:

Post a Comment