Monday, December 19, 2016

Hat-trick ya Ronaldo yaipa Madrid ndoo ya Dunia


Jana Jumapili December 18, Raeal Madrid imecheza dhidi ya Kashima Antlers kwenye bonge moja la fainali ya FIFA Club World Cup.
Wenyeji wa Kashima Antlers walikuwa vizuri tofauti na watu walivyokuwa wanawachukulia poa baada ya kuwabana washindi wa Champions League 2016 hadi dakika ya 90 ubao wa matokeo ulikuwa uanasomeka 2-2.
Game ikaelekea kwenye dakika za nyongeza na hapo ndipo Ronaldo akaamua mchezo.
Baada ya filimbi ya mwisho Madrid akawa mshindi kwa magoli 4-2.
Ronaldo amefunga hat-trick kwenye mchezo wa vilabu bingwa duniani. Bao la kwanza lilitokana na mkwaju wa penati baadae akafunga goli baada ya kuvunja offside trick ya Kashima na kuweka kambani.
Akamalizia hat-trick yake dakika ya 104 kwa shuti kali la karibu.

Source:shaffihdauda
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video



0 comments:

Post a Comment