Thursday, December 1, 2016

BODI YA DAWA NA VIPODOZI ZANZIBARA YAANGAMIZA TANI HIZI

Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeangamiza zaidi ya tani 62 za vyakula vibovu na vilivyopitwa na wakati katika zoezi lililofanyika Kibele Mkoa Kusini Unguja.

Mkuu wa Idara ya Biashara na Uendeshaji wa ZFDB Ndugu Abdulaziz Shaib  Mohd amesema bidhaa hizo mbovu zinatokana na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kujenga matumaini ya kuingiza faida kwa  bidhaa wanazouza bila kuangalia usalama wa bidhaa hizo kwa afya za watumiaji.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamiza bidhaa hizo, Ndugu Abdulaziz ambae pia ni Mkuu wa operesheni wa uangamizaji amesema bidhaa hizo zimegundulika kufuatia operesheni iliyofanywa na Bodi katika maghala na maduka mbali mbali ya Unguja  Sanjari kusema kuwa ZFDB ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi kwa matumizi ya wananchi, itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala yanayowekwa bidhaa na kwenye maduka ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa.


Mkuu wa Idara ya Chakula wa ZFDB bibi Aisha Suleiman amesema  mchango mkubwa wa raia wema ndio uliofanikisha kugundulika  bidhaa mbovu na zilizopitwa na wakati katika maduka na maghala mbali mbali Sambamba  kuwataka wananchi kujenga tabia ya kuchunguza tarehe ya kumaliza muda bidhaa wanazonunua na wanapogundua bidhaa imepitwa na wakati watoe taarifa katika Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi  ili hatua  za haraka ziweze kuchukuliwa.


Wakati huo huo Afisa Mkuu wa Idara ya Dawa na Vipodozi wa ZFDB Mwadini Ahmada Mwadini amesema vipodozi haramu vilivyokamatwa baadhi yake vinakemikali zenye sumu na hazifai kwa afya ya binadamu   sajari na kubainisha kuwa  Dawa zilizoangamizwa katika operesheni hiyo ni mafuta ya kula lita 10,105, sukari tani 2.15, mchele tani 26, tende tani 10, bidhaa  mchanganyiko za mboga mboga tani 13, dawa na vipodozi tania tatu.



Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video




0 comments:

Post a Comment