Saturday, November 5, 2016

YANGA WAKUBALI KUILIPA SIMBA MILIONI 200 ZA KESSY

HATIMAYE Yanga imekubali kuilipa Simba Sh milioni 200 kumaliza utata wa Hassan Kessy kudaiwa kuvunja mkataba na klabu yake ya zamani Simba.

Awali, Simba ilimlalamikia mchezaji Hassan Kessy kwa kuvunja mkataba na kudai kulipwa thamani ya mkataba ambayo ni zaidi ya dola laki sita, lakini baada ya mazungumzo Yanga wamekubali kulipa asilimia 10 ya mkataba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alisema Yanga iliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit na Simba iliwasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope.

“Pamoja na kutokuwepo kwa msuluhishi Said El-Maamry, haikuzuia pande hizo mbili kuendelea na mazungumzo, mazungumzo yalikuwa ni yenye mafanikio licha ya kutokuwepo msuluhishi”, alisema Lucas.

Lucas alisema walikubaliana kufika kikomo wikiendi hii kwa muda na sehemu wanayoijua wao ili waweze kumalizana kabisa kwa sababu wamekubaliana kuwekeza sehemu ili kulipa fidia na kumaliza utata wa kile ambacho Simba imekuwa ikikilalamikia.

Ili kuepuka suala hili kurudi kwenye kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji hawa viongozi wamekubali kumaliza na kuandika ripoti na kuileta TFF Jumatatu.

“Licha ya tofauti walizo nazo wanapokuwa uwanjani, na utani wao wa jadi ulivyo walikubaliani vizuri kuondoa utata na madai ambayo Simba iliwasilisha na kuona Yanga pakoja na Kessy walifanya makosa,” alisema Lucas.





Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video







0 comments:

Post a Comment