Thursday, November 10, 2016

TRUMP- NITASHIRIKIANA NA WAMAREKANI WOTE

Dakika chache baada ya Donald Trump wa Republican kutangazwa Rais wa Marekani, ametoa hotuba yake ya kwanza na kusema atashirikiana na Wamarekani wote.

Trump amesema tayari Hillary Clinton, amempigia simu kumpongeza kwa ushindi huo na kukubali matokeo.

“Nimepokea simu sasa hivi toka kwa Clinton, amenipongeza,” amesema na kuongeza:

“Ametupongeza sisi wote hapa, wote.”

Amesema hataacha kumsifu Hillary kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kampeni na kuwa alifanya kazi kubwa wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya nje.

“Alifanya kazi kubwa, tunampongeza…alifanya bidii sana” amesema

Kuhusu uchumi wa Marekani, Trump amesema amekuwa mfanyabiashara maisha yake yote hivyo atafanya kazi kubwa ya kuimarisha uchumi wa taifa kubwa la Marekani.

“Tutaimarisha miundombinu, biashara, viwanda na hakika tutaijenga upya Marekani,” amesema na kuongeza:

“Hakuna ndoto kubwa inayoshindikana, wala hakuna changamoto kubwa, tutaijenga Marekani pamoja”

 Ameishukuru familia yake, mke na watoto wake huku akiwatania kuwa baadhi ya watoto wake wana aibu lakini akasisitiza kuwa walimvumilia katika kipindi chote cha miezi 18 ya kampeni.

“Ilikuwa ngumu, ilikuwa ngumu,” amesema



Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video





0 comments:

Post a Comment