Wakati Paul Pogba akiwa anaungana na Eric Bailly, Chris Smalling na Antonio Valencia katika chumba cha matibabu, Jose Mourinho amefunguka na kusema kwamba sasa ni wakati wa kumrudisha Bastian Schweinsteiger katika kikosi cha kwanza.
Ile kauli ya muoshwa huoshwa imewakuta na vijana wa Man united jana baada ya kukubali kupewa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Fenerbahce.
Kocha Jose Mourinho anaona huu ndio utakuwa wakati sahihi kabisa wa kumrudisha Schweinsteiger katika kikosi chake baada ya Paul Pogba kuumia jana uwanjani na kuamua kutoka mchezoni.
Source: perfect255
0 comments:
Post a Comment