Friday, November 4, 2016

MAKONDA KUPANDA KIZIMBANI JUMATANO KUJIBU KESI YA MILIONI 200

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  Jumatano ijayo anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujitetea dhidi ya kesi ya madai ya Sh200 milioni  iliyofunguliwa na waliokuwa makada wa CCM, Mgana Msindai na John Guninita.

Makonda anayetetewa na Wakili wa kujitegemea Seneni Mponda, atatoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.

Msindai na Guninita wanatetewa na mawakili kutoka Kampuni ya Uwakili ya BM; Benjamin Mwakagamba na Ester Shedrack.

Katika kesi hiyo ya madai namba 68 ya 2015, Msindai na Guninita wanaiomba Mahakama kumuamuru Makonda awaombe msamaha na kumlipa kila mmoja Sh100 milioni.



Source: mtembezi.

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video






0 comments:

Post a Comment