Friday, November 11, 2016

Mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir afariki dunia alfajiri ya leo Dodoma


Mhe Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tannzaia  anasikitika kuwatangazia kuwa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo katika Hospitali ya General mkoani Dodoma.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae. Mhe Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.

Awali Marehemu pia alikuwa mwalimu wa soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa pamoja na waheshimiwa wabunge katika vikao.

Source:dewjiblog

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video



0 comments:

Post a Comment