Tuesday, November 8, 2016

MAPYA YAIBUKA VIDEO YA KALA JEREMIAH

Wakati mwingine inatakiwa sababu ambayo itamfanya mtu apate kitu ambacho kitamfanya afaidike au apate hasara, lakini video ya Kala Jeremiah imekuwa faida kwa familia moja hapa Tanzania.

Video ya “wanandoto” ambayo msanii huyo ameitoa imekuwa faida kwa familia ya mtoto aliyefahamika kama Adam, kwa maelezo ya mama wa Adam amesema kuwa alimpoteza mtoto huyo mwaka mmoja uliopita ambapo ilikuwa mwezi wa tisa mwaka jana, alitumia kila jitihada kumpata mtoto wake lakini ikawa ngumu kidogo.

Alipoona video ya Wanandoto ya Kala Jeremiah amefanya jitihada za kumtafuta msanii huyo ndipo akaenda katika kituo cha redio na  akampata Kala kupitia moja ya mtangazaji ndipo akawaunganisha.

Kilichotokea kumbe yule mtoto alikuwa katika kituo cha watoto yatima na alipotoa taarifa hapo wamethibitisha kweli alipatikana mwezi wa 9 mwaka uliopita na sasa mwaka mmoja taratibu za kumtafuta mzazi huyo zikaanza.

Hivi sasa mtoto huyo amepatikana na yuko katika mikono ya mama yake. Maelezo yake ameweka katika ukurasa wa Instagram wa Kala Jeremiah.



Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video








0 comments:

Post a Comment