Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anaendelea na ziara yake ya siku 10 katika wilaya Tano za Jijini humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majawabu yenye mlengo wa kuipata DARMPYA yenye matumaini kwa kila Mtanzania.
Moja ya maeneo aliyotembelea RC Makonda ni Kiwanda cha Water Com kinachojihusisha na uzalishaji wa maji na maziwa kilichopo Kisarawe wilaya ya Kigamboni, akiwa katika Kiwanda hicho RC Makonda amewataka watanzania kuwa wazalendo kwa kununua bidhaa za watanzania wenzao kwani kuna faida kubwa.
Akizitaja faidia hizo RC Makonda amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wazawa kuajiriwa katika viwanda hivyo na kutolea mfano kuwa kiwanda hicho kimeajiri zaidi ya watu 500,pia faida nyingine ni mapato kwa kiwanda binafsi kwa wazawa kununua vilevile kwa taifa kukusanya kodi kupitia viwanda hivyo, huku sababu nyingine ikiwa ni kutoa fursa ya uzalishaji wa malighafi kwa watanzania na kueleza kuwa kiwanda hicho kinazalisha lita 4000 za maziwa, kwa ukusanyaji wa maziwa nchi nzima wanakusanya lita 10000, na mashine zao zinauwezo wa kuzalisha lita zaidi ya laki mbili hivyo ni fursa kwa watanzania kuingia kwenye ufugaji wa kisasa na kujiongezea kipato.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha uzalishaji maziwa wa Milkcom Yusuph Said amesema wamejipanga kuzalisha lita milioni moja kwa siku, hivyo anawaomba watanzania waendelee kuwaunga mkono.
Source:mtembezi
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
0 comments:
Post a Comment