Balozi wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdulla Al Suwaid akizungumza na Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake leo Novemba 4.2016
Balozi wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdulla Al Suwaid mapema leo Novemba 4.2016 amemtembelea Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na kufanya mazungumzo. Moja ya mazungumzo waliyoongea ni pamoja na kuimarisha sekta ya afya ikiwemo ya kubadilishana kitaalam kwa kubadilishana ujuzi kwa madaktari wa nchi zote mbili
Katika mazungumzo hayo Waziri wa Afya mhe Ummy Mwalimu amemuomba Balozi wa Qatar kuishawishi Serikali yake kuanzisha Ushirikiano rasmi kati ya nchi hizi mbili katika Sekta ya Afya kwa kusaini Hati ya Makubaliano ya Kushirikiana.
Mhe Balozi amekubali Ombi la Mhe Waziri kwa kuahidi kulifanyia kazi. Ambapo maeneo ya ushirikiano ikiwemo kubadilishana kujenga uwezo wa Rasilimali Watu ikiwemo kubadilishana Wataalam na kuimarisha huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto ikiwemo upatikanaji wa Vifaa na Vifaa Tiba
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akifanya mazungumzo na Balozi wa Qatar , Balozi Abdullah Al Maadadi.
Aidha Waziri Ummy alimtaka Balozi huyo kusaidia Wilaya ambazo mapato yake ni kidogo na hawana hospitali za wilaya kuweza kuwajengea pamoja na kusaidia vifaa na vifaa tiba na masuala ya afya ya mama na motto nchini.
Hata hivyo Balozi Al Suwaid ameahidi kuisaidia Tanzania katika maeneyo yote aliyoyainisha Waziri pamoja na kuboresha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na ile ya matibabu ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akisalimiana na Balozi wa Qatar , Balozi Abdullah Al Maadadi.
Licha ya hivyp Balozi hiyo wamejenga kituo cha afya cha Waso kilichopo Wilayani Ngorongoro
Source: dewjiblog
0 comments:
Post a Comment