Tuesday, October 25, 2016

UN yaadhimisha miaka 71, yaahidi kuwezesha vijana


WAKATI Umoja wa Mataifa (UN) ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake, imeahidi kuwatumia vijana katika utekelezaji wa  malengo yake 17 ya maendeleo.
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez amesema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa  mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo.
“UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu kumi wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza,” amesema.



Read More.............




Source: dewjiblog

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video

0 comments:

Post a Comment