Tuesday, October 25, 2016

Mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa Dar (DSE) yapanda kwa asilimia 19


Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa wiki iliyopita kuishia Ijumaa ya tarehe 21 Oktoba 2016, zimepanda mara 19 zaidi kutoka laki 5 na kufikia 9.8millioni.
Afisa Masoko Mwandamizi wa DSE, Marry Kinabo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema kupanda kwa idadi ya hisa zilizouzwa kumechangia mauzo ya soko hilo kupanda kwa asilimia 28 kutoka bilioni 3 na kufikia 3.8 Billion.
Pia, amesema ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa 3.53% kutoka 20.8 trillioni hadi 21.56 trillioni, huku
Mtaji wa makampuni ya ndani ukipanda kwa asilimia 0.36 kutoka 8.13 trillioni hadi 8.16 trillioni.
Kinabo amesema sekta ya viwanda (IA) imepanda kwa pointi 26.16 kwa sababu ya kupanda kwa bei kwenye kaunta za TBL kwa 0.79%
Pia,Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) imeshuka kwa pointi 0.51 kwa sababu ya kushuka kwa bei kwenye counta ya DSE kwa 3.13%
Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali baada ya bei za hisa kwenye kaunta ya Swissport kubaki kwenye 3534.64
Pia Kinabo ametaja makampuni yanayoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kuwa ni benki ya CRDB kwa 95.18%, MKCB 2.92% na TBL kwa asilimia 0.79%.




Source: dewjiblog

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video

0 comments:

Post a Comment