Monday, October 3, 2016

Tunda Man asema amevutiwa kufanya muziki wa Singeli

Msanii wa muziki anayefanya vizuri na wimbo ‘Mama Kijacho’ Tunda Man ameuzungumzia muziki wa Singeli huku akihaidi siku moja ataingia studio na kuandaa wimbo wa Singeli.


Akizungumza na Bongo5 Jumapili hii, Tunda Man amesema muziki wa Singeli una ladha nzuri ndio maana umeweza kupendwa haraka na mashabiki wa muziki.
“Nimevutiwa kufanya muziki wa Singeli lakini naangalia program zangu kwa sababu kuna ngoma ambazo zipo na zinahitaji kutoka. Kwa hiyo ukifika muda ambao anaweza kufanya Singeli nitafanya kwa kuwa ni muziki ambao tayari umeshapendwa na una mashabiki wengi,” alisema Tunda.
Muimbiji huyo kutoka Tip Top Connection anajipanga kuachia wimbo wake mpya ‘Mwanaume Suruali’ hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment