Hatimaye nyasi bandia na vifaa vingine kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza vimewasili huku ujenzi huo ukitarajia kuanza rasmi leo, Jumatatu.
Mwenyekiti wa Chama Soka cha Mkoa wa Mwanza (MZFA), Jackson Songora alithibitisha kuwasili kwa makontena mawili yenye vifaa hivyo vilivyowasili juzi, Jumamosi.
Songora alisema kuwa vifaa vilivyowasili ni pamoja na nyasi bandia, magoli makubwa na madogo, gundi, trekta (kifaa cha kusafishia uwanja), nyavu na uzio.
Alisema kuwa tayari mkandarasi amemthibitishia ujenzi kuanza rasmi Jumatatu na kwamba anaamini ujenzi huo utakamilika kwa muda mwafaka.
Source: mtembezi
0 comments:
Post a Comment