Thursday, October 6, 2016

Moni wa Central Zone adai baada ya kuhamia Dar

Masanii wa muziki wa hip hop wa Kundi la Central Zone la Dodoma, Moni, amefunguka kwa kusema kuwa baada ya kuhamia Dar es Salaam ameanza kuona mafanikio katika muziki wake.


Rapper huyo ambaye mwaka huu alikuwa mmoja kati ya wasanii wapya waliopanda jukwaa la tamasha kubwa la muziki la Fiesta 2016, amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM kuwa ameanza kuona mafanikio katika muziki wake baada ya kuhamia Dar es salaam.
“Nayaona mafanikio katika muziki wangu baada ya kuhamia rasmi Dar kutoka Dodoma,” alisema Moni.
Rapper huyo amesema Dar es salaam ni sehemu ambayo inaweza kuwaongonisha wasanii na wadau mbalimbali wa muziki tofauti na ukiwa mbali na jiji hilo.
Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Vanilla & Strawbery’ ilioandaliwa Tongwe Record

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 

0 comments:

Post a Comment