Msanii mkongwe wa muziki, Inspekta Haroun baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Sharubu za Babu’ ulioandaliwa na Prince Dully Sykes, amerudi tena kwa producer huyo na kuandaa wimbo mpya ambao atauachia hivi karibuni.
Inspekta amesema Dully ni producer ambaye anaweza kutengeneza muziki wa kisasa ambao unakubalika na vijana wengi.
“Wakati bado nafanya maandalizi ya albamu yangu mpya pia napisha matamasha mbalimbali yaishe, hivi karibuni nitaachia wimbo wangu mpya ambao umeandaliwa na producer ambaye aliandaa ‘Sharubu za Babu’ Dully Sykes. Kwa hiyo mashabiki wangu wajue kuna mambo mengi mazuri yanakuja kutoka kwa Inspekta Haroun pamoja na albamu kama nilivyoeleza mwanzo,”
Pia alisema wimbo huo utatoka pamoja na video kabisa ili kukata kiu ya mashabiki wake wa muziki kwa upande wa video.
0 comments:
Post a Comment